Jumanne , 10th Oct , 2023

Afisa Habari wa JKT Queens Masau Bwire amesema malengo yao ni kutinga fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika kwa Wanawake inayotaraji kuanza Novemba 05, 2023 nchini Ivory Coast.

Akizungumza na EATV Bwire amesema kuwa licha ya kuwa wageni katika mashindano hayo Lakini katika kipindi hiki wamefanya maboresho makubwa kwa kusajili wa wachezaji wenyewe vipaji ambao watakwenda kuongeza nguvu kabla ya kwenda katika mashindano

"Hatuna hofu na kundi tulilopangwa nalo kwani tunaimani na kikosi chetu pamoja na benchi la ufundi lililopo kwa sasa,amesema  Masau Bwire.

Bwire amesema Kuwa uwanja wao wa Nyumbani wa CCM kambarage Mkoani Shinyanga umefungiwa na Bodi ya Ligi kuu Tanzania bara hivyo hivi karibuni watatangaza ni uwanja gani ambayo watautumia katika michezo yao.

kikosi cha JKT Queens kimepangwa Kundi A na Atletico FC ya Ivory Coast akiwa mwenyeji, Sporting Casablanca ya Morocco na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini ambao walitwaa ubingwa wa michuano hiyo 2021. JKT Queens ilipata nafasi hivo baada ya kushinda ubingwa wa Ligi ya Wanawake nchini  Tanzania na ubingwa wa CECAFA.