Jumatatu , 9th Oct , 2023

Winga Mbrazil Gabriel Martinelli amesema anaamini ushindi wa bao 1-0 walioupata dhidi ya bingwa mtetezi wa ligi kuu ya England Manchester City umeongeza hali ya kujiamini ndani ya kikosi hicho kwenye harakati za kugombea ubingwa wa EPL kwa msimu huu.

Martinelli aliyefunga bao hilo pekee mnamo dakika 86 amesema tunajua umuhimu wa kushinda kwenye michezo migumu tunayoicheza kwa sasa na kupata ushindi mbele yao inatuongezea hamasa na hali ya kujiamini.

Arsenal inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Epl wakiwa na alama 20 kwenye michezo 8 huku mara ya mwisho kupata ushindi dhidi ya Manchester City ilikuwa Disemba 2015 na kupoteza kwenye michezo 12 waliyokutana na City kwenye michezo iliyopita.