Jumanne , 3rd Oct , 2023

Mkufunzi Mauricio Pochettino amewaomba mashabiki wa Chelsea kuwa wavumilivu kwa wachezaji vijana ndani ya kikosi hicho baada kupata ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Fulham kwenye dimba la Craven Cottage Jumatatu ya Oktoba 02-2023

Pochettino amesema ni suala la muda,uvumilivu,kuamini wachezaji hawa vijana wenye vipaji huku tukiendelee kuwajengea kujiamini kuongezeka kwao na hili linahitaji  uvumilivu hata kama hatujapata matokeo kwenye michezo tunayoicheza mbeleni.

Chelsea inashika nafasi ya 11 kwenye msimamo wa Epl wakiwa na alama 8 kwenye michezo 7 waliocheza huku mchezo unaofuata watakuwa kwenye dimba la Turf Moor kupambana na Burnley inayofundishwa na mkufunzi Vincent Kompany Jumamosi ya Oktoba 07-2023.