Jumatano , 27th Sep , 2023

Takriban watu 100 wamefariki na wengine 150 kujeruhiwa baada ya moto kuzuka wakati wa harusi katika mji mkubwa wa Kikristo nchini Iraq.

Cheche  za  moto zilichochea moto huo, na kusababisha sehemu za dari kupata moto na kuanguka, maafisa wa moto walisema.

Mamia ya watu walikuwa wakisherehekea katika ukumbi wa karamu huko Qaraqosh katika jimbo la Ninawi wakati tukio hilo lilipotokea.Haijulikani ni nini kilichosababisha moto huo lakini baadhi ya ripoti zinasema kuwa fataki zililipuka.

Cheche  za  moto zilichochea moto huo, na kusababisha sehemu za dari kupata moto na kuanguka, maafisa wa moto walisema.

idara ya ulinzi wa raia ya Iraq imesema, ikinukuliwa na shirika la habari la serikali INA ikisema kuwa

Moto huo ulisababisha kuporomoka kwa sehemu za ukumbi kutokana na matumizi ya vifaa vya ujenzi vya gharama nafuu ambavyo vinaanguka ndani ya dakika chache wakati moto unapozuka,

Haikufahamika mara moja ikiwa bibi harusi na bwana harusi walikuwa miongoni mwa waathiriwa.

Picha za video zilizochapishwa mtandaoni zilionyesha wanandoa hao wakiwa kwenye sakafu ya densi kabla ya vipande vya moto kuanza kuanguka kwenye sakafu ya densi.

Maafisa wa zima moto walionekana wakipanda juu ya mabaki ya jengo hilo wakiwatafuta manusura siku ya Jumatano asubuhi.

.