
Watu saba wamepoteza maisha baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugonga lori lililokuwa limeharibika na kusimama barabarani katika Kijiji cha Kongo kata ya Bukwe wilayani Rorya, mkoani Mara.
Ajali hiyo imetokea alfajiri ya leo Septemba 11, wakati wakirejea kwao kutokea Tarime Mjini ambapo walienda jana jana Septemba 10 kutazama tamasha la Simba maarufu kama "Simba Day", walitokea Kijiji cha Utegi .
Wakiwa kwenye gari dogo aina ya Probox yenye namba za usajili T.625 DYV katikati ya Kijiji cha Kongo kata ya Bukwe wilayani Rorya waligongana na lori hilo na kupoteza maisha.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Tarime, Yonah Charles amethibitisha vifo vya watu hao akieleza kuwa alfajiri yaleo wamepokea miili ya watu saba watatu wakiwa wanawake na wanne wanaume wakiwa wamefariki kutokana na ajali. #EastAfricaTV