Akizungumza na Wanahabari, Afisa Habari wa Yanga SC, Ally Kamwe amesema wataingia na tahadhari kwenye mchezo huo na kugusia kuwa wachezaji wao wapo tayari kuandika historia.
"Tumesikia kauli za Kocha wa Al-Merrikh anasema kuwa Young Africans inaogopeka Afrika. Sisi tumesoma Cuba, tunamwelewa, hawezi kutuchota, tutauchukulia mchezo wetu wa pili kwa umakini mkubwa.
Amesema pia anakuja kufunguka hapa, kwetu sisi ni taarifa njema kwa sababu mnara haukusoma Rwanda, hivyo tukipishana nao itakuwa fursa ya kusimamisha mnara" Kamwe amesema
Vile vile Kamwe amewaomba mashabiki na Wanachama wa Yanga SC kujitokeza kwa wingi kwenye dimba la Chamazi kuwaunga mkono kwani Jumamosi hiyo ni siku ya Stephane Aziz Ki.
"Ukitaka kujua wana Yanga wana ugwadu na huu mchezo, tayari baadhi yao wameshaingia kwenye mfumo kuangalia tiketi, Tayari baadhi ya mashabiki wameshanunua tiketi kupitia mfumo kabla ya sisi kutangaza mfumo hadharani.
"Sisi sio Klabu namba tatu kwa ubora wa Afrika kwa bahati mbaya, ni lazima tuonyeshe hilo kwa kutinga hatua ya makundi. Hivyo hizi tiketi zinaweza kuisha mapema mno kama shabiki hutanunua tiketi mapema"Kamwe amesema
Yanga SC ina faida ya magoli 2-0 waliyoyapata kwenye mchezo wa kwanza, hivyo Jumamosi ya Septemba 30, 2023 inahitaji sare yeyote, ushindi au isifungwe magoli zaidi ya 2 ili kutinga Makundi ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika mwaka 2023-24.