Ijumaa , 22nd Sep , 2023

Aliyekuwa Makamu wa Rais wa Simba SC, Geofrey Nyange Kaburu amesifu usajili waliofanya katika timu yao licha ya kikosi hicho kutokuwa na muunganyiko mzuri katika mechi mbalimbali ambazo wameshashuka dimba msimu huu wa mwaka 2023-24.

Akizungumza na EATV, Kaburu amesema kuwa kikosi hicho bado hakijafikia ubora ambao mashabiki wanatarajiwa kuuona hivyo kikosi hicho kinahitaji muda wa kukaa pamoja ili kipate muunganiko zaidi.

''Tutoe muda kwani kikosi ni kizuri kwa mchezaji moja ambae amesajiliwa huu ni mwanzo tu naamini wakipata mechi nyingi zaidi ya kucheza  na kuzoeana basi wachezaji wote wataingia ndani ya mfumo’’amesema Kaburu.

Aidha Kaburu ameipa nafasi timu yake ya Simba SC kufanya vizuri kwenye mchezo wa Ufunguzi wa mashindano ya African Football League dhidi ya Al Ahly unaotaraji kutimua vumbi Oktoba 20, 2023 katika uwanja wa Benjamin MKapa, Jijini Dar es salaam.

Kikosi cha Simba SC jana Septemba 21, 2023 kilishuka dimba dhidi ya Coast Union ya Tanga kwenye Mchezo wa Ligi kuu NBC Tanzania uliochezwa katika dimba Uwanja wa Uhuru jijini Dares Salaam na kuibuka ushindi wa bao 3-0 kuifanya timu hiyo kufikisha alama 9 sawa na vinara wa Ligi Yanga SC lakini Mabingwa hao watetezi wakiwa na idadi kubwa ya mabao ya kufunga, mabao 11