Alhamisi , 21st Sep , 2023

Mtoto wa kiume wa Rais wa Nigeria Bola Ahmed Tinubu aitwaye Seyi Tinubu ametoa kiasi cha fedha N15 milioni Tsh 48,621,000 kwa mtoto wa marehemu Mohbad.

Kushoto ni Mohbad na mtoto wake, kulia ni mtoto wa Rais wa Nigeria

Akaunti hiyo imefunguliwa kwa ajili ya mtoto wa marehemu ili kusaidia familia ambayo Mohbad aliiacha. Hadi sasa zaidi ya N35 Milioni sawa na Tsh 113,449,000 ambazo zimeshatolewa.

Mohbad alifariki Septemba 12 na raia wa Nigeria wametaka uchunguzi  wa mwili wake ufanyike kufuatia chanzo cha kifo chake huku lebo aliyowahi kufanya nayo kazi Marlian Music kuhusishwa kwenye kifo hicho.