Jumatano , 20th Sep , 2023

Chama cha soka mkoa wa Ilala 'IDFA' kimefungua kozi ya siku kumi ya makocha kwa ngazi ya CAF Diploma C ambayo inashirikisha washiriki 32 kutoka Tanzania bara na Visiwani.

Akifungua Mafunzo hiyo makamu mwenyekiti wa chama cha Soka mkoa wa Dar es salaam  DRFA Ben Kisaka amewataka yale yote yanayofundishwa kuyazimgatia ikiwemo kuwa na maadili mema katika sehemu za kazi.

“Kozi hizi zinasaidia katika kuzalisha waalimu wengi ambao watakwenda mtaaani katika kusaka  kuibua  vipaji ambavyo vinaweza kusaidia taifa siku zijazo “amesema Kisaka Makamu mwenyekiti DRFA.

Nae mwenyekiti wa chama cha soka Mkoa wa Ilala Mussa Kondo ameleezea umuhimu wa kozi hiyo kwa washiriki huku kozi hiyo itafungwa rasmi Septemba 27,2023 mwaka huu jijini Dar es salaam.

“kozi kama hizo ni moja ya vipaumbele vyangu   vya kuzalisha Makocha wengin Tanzania bara na Visiwani”amesema Kondo.

Nao washiriki wa kozi hiyo ya  CAF Diploma C wamesema Mafunzo hayo yatawasaidia wao kuwa makocha wazuri na wenyewe weledi.