
Soko hili la Mlango mmoja ni miongoni mwa maeneo ya biashara jijini Mwanza yenye mkusanyiko mkubwa wa watu ambapo wafanyabishara zaidi ya 1000 hufanya kazi zao hapa, lakini hofu ya wafanyabiashara hawa ni watoto wanaokadiriwa kuwa na umri kati ya miaka miwili hadi mitano ambao wamekuwa wakirandaranda sokoni hapa wakati wa kazi jambo ambalo sio salama kwao.
Kwa upande wao baadhi ya kinamama wanaeleza sababu za kuja na watoto wao katika maeneo hayo ya soko, akiwemo mama huyu ambaye hakutaka jina lake litajwe ambaye anasema miongoni mwa sababu ni wanaume kuwaachia wanawake suala la malezi ya mtoto.
'Kinababa warding kwenye majukumu yao wamwogope mwenyezi Mungu watoto wanapata shida humu. Inamaana kule nyumbani tunashindwa kuwaacha kwa sababu ya usalama.'
Naye mwenyekiti wa soko hilo Jackson Antony amesema wameshatoa elimu kwa wazazi hao kutokuja na watoto lakini kutokana na changamoto hiyo kuendelea wanaiomba serikali iwasaidie ili kutafuta ufumbuzi.