Jumatano , 13th Sep , 2023

Jeshi la Polisi mkoani Mtwara linaendelea na uchunguzi wa kifo cha binti mlemavu wa mikono na miguu aliekutwa amefariki nyumbani kwao mwili wake ukiwa umefungwa kamba shingoni kama kajinyonga.

Sehemu aliyojinyongea

Tukio hilo limetokea katika mtaa wa Sinde Msanga Mkuu, binti mlemavu wa miguu na mikono aitwaye Samia Mohammed aligundulika amefariki huku mwili wake umevuja damu mdomoni na puani na akiwa amefungwa kamba ya manila shingoni mwake kama kajinyonga.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mtwara ACP Mtaki Kurwijila ameeleza katika upelelezi wa awali wamebaini yakwamba kutokana na ulemavu wa mikono na miguu aliokuwa nao marehemu uwezekano wa yeye kujinyonga ni mdogo sana na hivyo wanaendelea na uchunguzi wa kina ambapo wanamshikilia babu yake na marehemu.