Jumanne , 12th Sep , 2023

Jumla ya watahaniwa 1,397,370 wa darasa la saba nchini, wataanza kufanya mitihani yao ya kumaliza elimu ya msingi kuanzia kesho Septemba 13 hadi 14, 2023.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Dkt. Said Mohamed

Taarifa hiyo imetolewa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Dkt. Said Mohamed, na kusema kati ya watahiniwa hao, 654,652 ni wavulana wasichana ni 742,718.

Ambapo wasimamizi wote walioteuliwa kusimamia mitihani, wasimamie mitihani kwa makini na uadilifu wa hali ya juu na wazingatie kanuni za mitihani na miongozo waliyopewa ili kila mtahiniwa apate haki yake.

"Mwanafunzi yeyote atakayebainika kufanya udanganyifu matokeo yake ya mtihani yatafutwa kwa mujibu wa kanuni za mitihani, wamili na wakuu wa shule baraza linawataka shuwatambue shule zao ni vituo maalum vya mitihani hawatakiwi kuingilia majukumu ya wasimamizi wa mitihani, baraza halitosita kukifuta kituo cha mitihani endapo litajiridhisha pasipo shaka kuwa uwepo wake unahatarisha usalama wa mitihani ya Taifa," amesema Katibu Mtendaji wa NECTA