Alhamisi , 24th Aug , 2023

Mkuu wa kundi la mamluki la Wagner Yevgeny Prigozhin anadhaniwa kuwa aliuawa katika ajali ya ndege kaskazini mwa Moscow, pamoja na mtu wake wa  karibu Dmitry Utkin na wengine wanane.

Rais Volodymyr Zelensky ameliambia shirika la habari la Interfax-Ukraine kwamba Ukraine haikuhusika katika kifo cha bosi wa Wagner Yevgeny Prigozhin

Ndege hiyo inayomilikiwa na Prigozhin, ilikuwa na abiria saba na wafanyakazi watatu wakati ilipoanguka katika eneo la Tver. Miili yote 10 imepatikana, ripoti zinasema

Kufuatia ajali hiyo na vifo hivyo kumekua na mshangao baada ya Rais wa Urusi Vladimir Putin wa Urusi  kutotaja ajali hiyo wakati akihutubia mkutano wa kimataifa kwa njia ya video.

Hata ikulu ya Kremlin bado haijasema lolote kuhusu ajali ya ndege ya Jumatano ambapo kiongozi wa Wagner Yevgeny Prigozhin anadhaniwa kuwa amefariki dunia.

Kuna uvumi mkubwa juu ya kile kilichotokea. Vyanzo vya ulinzi vya Uingereza vinaiambia BBC kuwa shirika la ujasusi la Urusi FSB lina uwezekano mkubwa wa kuwajibika.

Wakati huo huo , Rais Volodymyr Zelensky ameliambia shirika la habari la Interfax-Ukraine kwamba

Ukraine haikuhusika katika kifo cha bosi wa Wagner Yevgeny Prigozhin. Rais huyo amesema nchi yake haijahusika na suala hilo na kwamba  anatambua ni nani ana uhusiano na suala  hilo