Jumanne , 22nd Aug , 2023

Wananchi katika Kijiji cha Izindabo kata ya Lugata kisiwa cha Kome Wilayani Sengerema mkoani Mwanza wameishukuru serikali kupitia Taasisi ya wanyamapori (TAWIRI) katika oparesheni ya vuna mamba kwa kufanikisha kumuua mamba aliyekuwa akitishia uhai wa wakazi hao

Wakazi hao wameeleza furaha yao baada ya kuuawa kwa mamba huyo, ambapo wamesema amekuwa akiwaletea athari kubwa ikiwemo kusababisha vifo suala lililowafanya waogope kuchota maji ziwani na kupelekea kukosa huduma za muhimu

Hatua ya TAWIRI kuanzisha oparesheni vuna mamba imekuwa tumaini kwa wakazi wa maeneo hayo kwa kusaidia kuuawa kwa mamba mmoja aliyekuwa kero kubwa kisha kugawiwa kwao kama kitoweo