Taarifa hiyo imetolewa na Afisa habari wa Yanga SC Ally Kamwe kuwa majina yote ambayo benchi la ufundi waliwasilisha katika ofisi ya mtendaji wa Yanga SC yameshapelekwa hivyo mashabiki wasiwe na presha kwani kila mchezaji waliyemuona hatatumika katika mashindano.
“Wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri hatuna majeraha hadi muda huu hivyo tunasubiri kwenda mkoani Tanga kwenda kuchukua kombe letu “amesema Ally Kamwe.
wakati huo huo Kamwe ametoa pongeza kwa klabu zote zinazoshiriki Ligi kuu NBC Tanzania msimu ujao kwa kufanya usajili mzuri na wenyewe kutoa ushindani katika Ligi yetu .