Akizungumza Dar es Salaam Alhamisi ya Julai 27,2023 , wakati wa hafla ya utiaji wa Saini wa mkataba wa uwanja wa Benjamini Mkapa Waziri wa Utamaduni ,Sanaa na Michezo Balozi Dkt Pindi Chana, amesema hayo ni chachu ya mafanikio ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kutokana na uwekezaji wake.
"Kukarabati uwanja ni muhimu kwa sababu umetengenezwa muda mrefu tangia mwaka 2005 hadi leo hii, pia tutaendelea kufanya marekebisho ya viwanja vingine saba hapa nchini "amesema Pindi Chana
Naye Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Said Yakubu amesema fedha hizo zitatumika Katika maboresho Katika vyumba vya kubalishia wa chezaji ,kubadilisha viti, vya uwanja, mfumo wa matangazo,ubao,wa kidigitali.
"Maboresho yanalengo kuhakikisha uwanja wetu uendelee na kukidhi vigezo vya FIFA na CAF na sasa unatambulika kimataiafa na tunaahidi matunzo ya uwanja utakapokamilika yatakuwa bora kuliko miaka 16 iliyopita ," amesema Yakubu.
Kwa upande Makamu wa Rais wa pili Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Steven Mguto,alisema shirikisho Katika uboreshaji wa Uwanja huo itajenga benchi la ufundi na wachezaji wa ziada na tayari wamekabidhi mchoro huo.