
Picha za kutoka msitu wa Shakahola
Mratibu wa usalama Kaunti ya Mombasa Rhoda Onyacha amesema kwamba maafisa wanaoshughulikia ufukuaji wa miili ya Shakahola waliko wafuasi wa mhubiri Paul Makenzi, wanaoendeleza ibada ya kufunga hadi kufa sasa imefikia 419.
Aidha watu waliookolewa mpaka sasa ni 95, na washirikishi wa Makenzi 37 wanashikiliwa na vyombo vya usalama na shughuli ya kutafuta makaburi na kuyafukua bado inaendelea.