Ijumaa , 20th Jun , 2025

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amezindia mradi wa Maji Butimba uliopo eneo la Butimba Jijini Mwanza ambao umegharumu Tzs Bilioni 71.6.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amezindia mradi wa Maji Butimba uliopo eneo la Butimba Jijini Mwanza ambao umegharumu Tzs Bilioni 71.6.

Mradi wa huo umetekelezwa kwa ushirikiano baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Washirika wa Maendeleo ambao ni Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (European Investment Bank - EIB), Shirika la Maendeleo la Ufaransa (Agence Francaise de Développement - AFD) na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU) chini ya programu ya “Lake Victoria Water and Sanitation (LVWATSAN)”.

Aidha, Mradi huo una uwezo wa kuzalisha Lita za maji Milioni 48 kwa siku na utanufaisha wananchi zaidi ya 450,000 wa Wilaya za Nyamagana, Ilemela na baadhi ya maeneo ya Wilaya ya Magu.

Mradi wa MAJI BUTIMBA umetekelezwa kwa gharama ya TZS. 71,696,908,539.00 na hadi sasa maeneo ya Nyegezi, Mkolani, Buhongwa, Nyamazobe, Nyahingi, Buganda, Luchelele, Lwanhima, Sahwa, baadhi ya maeneo ya Fumagila, Kishiri, Igoma, Nyamhongolo , Kisesa na Bujora yananufaika na maji kutoka katika chanzo hicho.

Upatikanaji wa huduma ya maji kwa sasa Jijini Mwanza umefikia asilimia 87 na hivyo kufikia lengo la Serikali la kufikia asilimia 85 za upatikanaji wa huduma ya maji Mijini.