Jumanne , 16th Jun , 2026

Kwenye moja ya mahojiano, mwandishi wa habari alimuuliza Maldini iwapo Messi alikuwa na bahati ya kutokutana naye uwanjani kabla Maldini hajastaafu soka, kwani Messi alikuwa majeruhi wakati AC Milan ilipocheza na Barcelona.

Mwandishi: "Je, Messi alikuwa na bahati ya kutocheza dhidi yako kwa sababu alikuwa majeruhi?"

Paolo Maldini alijibu:
"Hapana, hapana. Mimi ndiye niliyepata bahati sikucheza dhidi ya Messi kwa sababu alikuwa majeruhi, namshukuru Mungu alikuwa majeruhi."

Hiyo siyo taarifa, taarifa ni kwamba

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Argentina, Lionel Scaloni, amethibitisha rasmi kuwa nahodha wake na bingwa mtetezi wa Kombe la Dunia, Lionel Messi, yuko fiti kwa 100% na ataanza kwenye mchezo wa kwanza wa ufunguzi wa Kundi J wa mashindano ya FIFA World Cup 2026 dhidi ya Algeria.