
Hii ni baada ya wizara ya madini kukamilisha utafiti wa kiwango chake uliofanyika kijiji cha Kinangali ambayo imeelezwa kuwa ina ubora
Imeelezwa kuwa wingi wa chumvi katika mbuga hiyo imekadiriwa kufikia tani milioni 46.
Wananchi hao wamezungumza katika kijiji hiki cha KINANGALI wilaya Manyoni mkoani Singida, wanaiomba serikali kuwasaidia kuboresha bei ili waweze kutengeneza chumvi kwa ubora zaidi.
Katika kuhakikisha utunzaji wa mazingira diwani wa kata hiyo Samwel Ligoha anatilia mkazo wa uwezeshwaji wa kutumia tekonolojia ya kisasa. ikiwemo umeme na makaa ya mawe katika na kuongeza uzalishaji wenye tija.
Kufuatia agizo la Naibu Waziri wa Madini la kuwataka wanajiojia kufika katika mbuga hiyo kufanya utafiti wa aina ya madini chumvi hiyo, wamewasilisha ripoti kwa mkuu wa wilaya Manyoni