
Akizungumza na waandishi wa habari amebainisha kuwa jamii inapaswa kutambua umuhimu wa uchangiaji wa damu kwakuwa uhitaji wa damu ni mkubwa hivyo wadau mbalimbali wanatakiwa kuendelea kujitokeza katika uchangiaji wa damu.
Aidha, Mkuu wa Wilaya amesema kutokana na takwimu ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 wilaya ya ubungo ina watu wapatao takribani Milioni 1 hivyo kufanya uhitaji wa damu kuwa mkubwa.
Kupitia kampeni mbalimbali za uchangiaji wa damu zinazoendelea nchini, Mkuu wa wilaya amebainisha kuwa wilaya ya ubungo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imekusudia kupata takribani chupa 311 kupitia kampeni ya USAID Afya yangu kwa kushirikiana na Hananja Compasion Foundation.