Jumapili , 18th Jun , 2023

Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo amewaagiza Mawaziri wa Wizara ya Kilimo na Wizara ya Fedha na Mipango, kukutana na kujadili namna ya kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ya kilimo ambayo imeanzishwa na serikali ili ikamilike ndani ya muda uliopangwa na tija yake ionekane kwa wananchi.

Kushoto ni Waziri wa Fedha Dkt Mwigulu Nchemba, na kulia ni Waziri wa Kilimo Hussein Bashe

Ndugu Chongolo amesema hayo leo Juni 18, 2023 baada ya kukagua mradi wa Umoja wa Wakulima wa Zabibu wa ICHIMADA ulioko eneo la Chinagali, pamoja na Mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji wa ‘Jenga Kesho Iliyo Bora' (BBT) uliopo katika eneo hilo wilayani Chamwino mkoani Dodoma. 

Katibu Mkuu Chongolo amesema kuwa dhamira ya  Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan,ni kuona miradi ya kilimo inaleta tija kwa haraka, hivyo ni muhimu miradi hiyo isiwe na majina mazuri tu, bali ilete matokeo na manufaa kwa wananchi.