
Wakazi wa eneo hilo wameomba serikali kuliangalia eneo hilo kutokana na kukosa matuta na alama za kusaidia kuitakbuliaha kuonesha kona hiyo.
Wakizungumzia ajali hiyo iliyotokea jana mchana eneo la Yombo mwisho wa Lami mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Machimbo Rahim Maridadi pamoja na baadhi ya wananchi wa eneo la Yombo wamesema tukio hilo limetokea jana
mchana ambapo lori hilo likiwa katika hali ya mwendokasi lilimshinda dereva na kudondosha kontena ambalo lilipelekea majeruhi na kifo cha mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Bahati Christandus .
Mganga mfawadhi wa hospitali ya Temeke Dkt. Joseph Kimaro amethibitisha kupokea majeruhi wanne na mwili mmoja ambapo majeruhi hao akiwemo mtoto mdogo ambaye ni mtoto wa marehemu Bahati aliyeokolewa na mama yake wakiwa wanaendelea vyema .
Nyumbani kwa marehemu Bahati Christandus baahi ya majirani na ndugu wa marehemu wameendelea kuombeleza huku msemaji wa familia Gabriel Mtole amethibitisha mtoto aliyejeruhiwa kuwa ni mtoto wa marehemu na aliumia baada ya mama yake kumrusha ili amuokoe kufuatia ajali hiyo.