Jumanne , 13th Jun , 2023

Rais wa Gambia Adama Barrow, ambaye alichaguliwa tena mwaka 2021, amedokeza kwamba huenda akagombea muhula wa tatu katika uchaguzi ujao wa 2026.

Gambia haina ukomo wa mihula ya urais na marais wawili wa zamani wote walihudumu kwa zaidi ya miongo miwili madarakani. Wakati wa mkutano kaskazini mwa nchi hiyo Rais Barrow alisema wale wanaomsubiri aachie madaraka wanapaswa kusubiri kwa muda mrefu zaidi.

Kiongozi huyo wa Gambia alidai kuwa kuna watu wanazunguka wakiwaambia raia wa Gambia kwamba anataka kuachia madaraka na kwamba hivi karibuni wataidhibiti serikali. Alisema kuwa haendi popote.

Bwana Barrow aliingia madarakani mwaka 2017, kwa makubaliano kwamba atahudumu kwa miaka mitatu tu na kisha kuachia madaraka - lakini alikaidi ahadi hiyo ya kampeni.

Katiba mpya iliyotungwa mwaka 2019 ilijumuisha ukomo wa mihula miwili lakini haikupitishwa na bunge.