Jumapili , 11th Jun , 2023

Kuelekea mcheoz wa fainali Kombe la Shirikisho ASFC kati ya Yanga na Azam FC, kocha Nasreddine Nabi amezungumzia sababu ya kuwakosa Fiston Mayele na Stephane Aziz-Ki.

Kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi na mastaa Fiston Mayele, Stephane Aziz-Ki

Kocha Nabi amesema kuwa sababu ya kuwakosa mastaa hao ni mashirikisho yao soka ya nchi zao kukataa ombi la Yanga kuendelea kuwatumia kwenye mchezo huo wa fainali.

"Awali tulikuwa tuwakose Djigui Diarra, Kennedy Musonda na Khalid Aucho lakini mashirikisho ya mpira ya nchi zao yameturuhusu kuwatumia kesho bila shida lakini Mayele Fiston na Aziz Ki mashirikisho yao yamekataa ombi letu hivyo hatutokuwa nao’’, amesema kocha Nabi.