
Akizungumza na mamia ya wananchi wa mji wa Kibaya katika mkutano wa Chadema Godbless Lema amesema siasa ni chimbuko la maendeleo
"Katika nchi kama hii wananchi ambao ni maskini, wanashida ya maji watoto wao wana tatizo la elimu na afya unapoita mkutano wa kisiasa kama huu tusione udogo kwa sababu siasa ni maisha yenu" amesema Lema
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameteua wakurugenzi wa halmashauri na kuhamisha wengine vituo vya kazi sambamba na makatibu tawala
"Leo mama Samia ameteua wakurugenzi na makatibu tawala wilaya na hapa Kiteto mmeletewa mkurugenzi mpya.. mlikuwa na mkurugenzi mmoja wa ajabu ajabu sana alikuwa anatisha tisha watu na madiwani na ana bahati ameondoka nilikuwa nakuja kuweka kambi hapa" amesema Lema
Mwenyekiti Chadema mkoa wa Manyara Dr Deriki Magoma amezungumzia huduma ya afya huku Ramadhani Mwamba akieleza hali ilivyo sasa kuhusu huduma ya afya Kiteto
"Sasa hivi viongozi wote ni CCM, kuanzia Rais wabunge madiwani wote hao wanatoka na CCM je hali ya maisha ya wananchi yamebadilika huduma zijoje?
"Kwenye zahanati hapo Bwagamoyo ambayo ina hudumia wananchi karibia mji mzima wa Kibaya tulisema hivii watu wachangie sh 3000 leo hii ukienda ni sh 7000 ni hasara hii inayotokana na uwakilishi wa upande mmoja"Ramadhani Mwamba Mwenyekiti wa Chadema Kiteto
"Tunahitaji katiba mpya Tanzania itakayo jibu shida za watu sio kitabu kipya"