
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo Julai 1/2025, imeahirisha tenaKesi ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu mpaka Julai 15/2025, kwa ajili ya kutolea maamuzi kama itapelekwa Mahakama Kuu au shauri hilo litafutwa.
Maamuzi hayo yametolewa na Hakimu Mfawidhi Franko Kiswaga Mara baada ya majibizano ya kisheria baina ya mawakili upande wa Jamhuri pamoja na mshtakiwa ambaye alikuwa akijitetea mwenyewe na kusema kuwa Julai 15, Mahakama itaamua hatma ya shauri hilo.