Tayari kampuni nne zimejitokeza kununua kwa wastani wa bei ya kitaifa ya dola mbili kwa kilo
Wakizungumza na EATV katika uzinduzi wa soko la tumbaku msimu wa kilimo 2022/2023 iliyofanyika kata ya Mitundu halmashauri ya Itigi wilayani Manyoni mkoani Singida, wakulima hao wamezungumzia fursa ya kilimo hicho kwa kuwa miaka kadhaa iliyopita kilimo hicho kilionekana kusuasua kutokana na kukosekana kwa masoko.
Kutokana ongezeko la bei vyama vya ushirika vitanufaika na kutoa hamasa kwa wakulima kuendelea kulima ziadi katika msimu ujao kama anavyosema Anasia Kimambo meneja wa chama kikuu cha ushirika na na masoko kanda ya kati
Kwa upande wao wanunuzi kutoka kampuni ya Alliance one na Magefa wanasisitiza wakulima kuingiza mazao yao sokoni mapema ili kupata mdaraja yenye ubora na kupata motisha.
Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa wilaya Manyoni afisa tarafa ya Itigi Eliuta Kidenya amewataka wakulima hao kupeleka tumbaku bora badala ya kuchanganya na vitu visitakiwa kwa lwngo la kuongeza uzito katika kilo.