
Wakizungumza na #EATV wananchi hao wamekishukuru kituo hiki kwa kuripoti habari hiyo na serikali kuona na kwenda kuweka matuta manne ambayo sasa wamesema yamesaidia kupunguza mwendo wa vyombo vya usafiri vinavyotumia barabara hiyo
Hata hivyo mmoja wa viongozi wa wananchi hao amesema #EATV imefanya jitihada kubwa ambazo zimesaidia serikali kufahamu changamoto iliyopo katika mtaa huo kwani ajali hizo zilizokuwa zinatokea zimekuwa zikihatarisha usalama wa maisha ya wananchi
Hata hivyo mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Tandale Muhalitani amewataka madereva wa vyombo vya moto wananitumia barabara hiyo kuacha kuendesha vyombo hivyo kwa mazoea kwani madereva wengi hasa wa bodaboda wamekuwa wakianguka kutokana na kutotanbua kama barabara hiyo tayari imeshawekwa matuta
EATV imefanya jitihada za kumtafuta meneja wa wakala wa barabara mijini na vijijini wilaya ya Kinondoni ili kuzungumzia suala hilo la uwekaji matuta lakini jitihada hizo zimegonga mwamba baada ya simu yake kuita bila kupokelewa