Jumamosi , 14th Feb , 2015

Msani mkongwe wa muziki hapa Tanzania, Mzee Ally Zahir Zorro amesema kuwa, mpango wake wa mwaka jana wa kujenga hostel ya kisasa kwa ajili ya Bendi yake ya muziki kwa sasa umesimama kidogo.

Zahir Zorro

Zahir amesema mpango huo umesimama akiwa ameelekeza nguvu katika kuiimarisha bendi yake mpya, kabla ya kuendelea tena na shughuli hiyo.

Mzee Zorro amesema kuwa, mpango huo wenye lengo la kuileta bendi hiyo kwa pamoja, amekua akiufanya kwa mwaka mzima sasa na kutokana na hali halisi na ushauri wa familia ameamua kuusitisha ujenzi wa hostel mpaka hapo baadaye, akitumia muda huu wa sasa kuhakikisha bendi inakwenda.