
Makamba ametoa maelekezo hayo wakati wa hafla ya kukabidhi rasmi kibali Cha Ujenzi wa mradi wa Bomba la kusafirisha mafuta Kwa Kampuni ya EACOP inayotekeza mradi huo ambao unapita kwenye mikoa nane ya Tanzania hara ikiwemo Kagera,Geita,Shinyanga, Singida,Tabora Dodoma na Manyala
Amesisitiza kuwa mradi huo umezingatia mikataba yote ya utunzaji wa mazingira na haki za binadamu hivyo ni lazima utekelezwe kwasbaabu unamanufaa makubwa ya kichumi katika nchi ya Tanzania na mataifa jirani Mradi huo unatarajiwa kukamilika ndani ya miaka mitatu ambapo shughuli za awali zimeshaanza kufanyika na mradi muhimu Kwa Tanzania ukigharimu Dola za kimarekani bilioni 4.5
Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Dkt James Andelile amesema baada ya kufanya tathmini ya kina kuhusu mradi huo mamlaka hiyo imejiridha ndiyo maana imetoa kibali rasmi Cha kuruhusu kuanza utekelezaji wa unezi wa Bomba la kusafirisha mafuta Kwa kipande Cha Tanzania kutoka Mtukura Hadi Chongoreani Tanga
Mradi huo unatarajiwa kukamilika ndani ya miaka mitatu ambapo shughuli za awali zimeshaanza kufanyika na mradi muhimu Kwa Tanzania ukigharimu Dola za kimarekani bilioni 4.5
Katika halfa hiyo imebainishwa kuwa Tayari shilingi bilioni 29 imeshatumika kulipa fidia Kwa wakazi waliopitia na mradi huo na taratibu za kufioa fidia zinaendelea hivyo serikali imewatoa hofu wote watakaopitiwa na mradi huo kuwa wataoata stahiki zao kikamilifu