Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu za Serikali (NBAA), Profesa Sylivia Temu, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wahasibu Duniani.
“Tuzingatie uzalendo na maslahi ya taifa lakini pia nimewaasa tusijifungie kwasababu dunia imekuwa kama kijiji hivyo tujipange tuwe na mtazamo mpana ili tuweze kufanyakazi za kimataifa kama Umoja wa Mataifa,” alisema
“Nimewaambia wahasibu kwamba tumeshaandika hadithi ya miaka 50 iliyopita sasa tujiulize miaka 50 ijayo tunafanya nini ili tuwe endelevu tusiwe wale wale tu tunatakiwa kwenda sanjari na mabadiliko,” alisema
Aidha, alisema bodi ya NBAA imeshaanza kuonyesha mfano kwa kufanya kazi za kihasibu kimataifa ambaapo wameanza kutoa ushauri nchini Msumbiji na Malawi na wanatarajia kwenda kwenye mataifa mengine.