Jumatano , 2nd Nov , 2022

Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania hii leo imezindua huduma ya kupata habari kwa haraka na unafuu wenye bei rahisi zaidi kupitia program mpya ya E gazzete ambayo sasa ukiwa na app hiyo itakuwezesha kupata habari maudhui na huduma kwa njia ya mtandao bila kubagua mtu.

Akizindua huduma hiyo Mkurugenzi wa kidijitali kutoka vodacom Nguvu Komando amesema ni muda mwafaka ambao sasa watanzania zaidi ya milioni 17 wanatarajiwa kufikiwa na huduma hii ambayo imejaa maudhui ya ndani.

Huduma hiyo ambayo Vodacom imeizindua pamoja na mwananchi sasa kupitia kasi ya mtandao wa 5g wito umetolewa kupakua my vodacom app ili kupitia taarifa zote za siku lengo ikiwa kupata msingi wa maendeleo kupitia njia ya kidigitali.