
Wamachinga
Wakizungumza na EATV leo Oktoba 24, 2022, viongozi hao wamesema zaidi ya wafanyabiashara 200 wamekimbia kwenye masoko ya machinga yaliyopo katika wilaya hiyo na kwenda barabarani.
Kwa upande wake Rashidi Shabani ambaye ni Mwenyekiti wa wafanyabiashara Machinga Complex, ameitaka serikali kuwa na kanzidata ya wafanyabiashara wadogo ambayo itasaidia kuipa serikali urahisi wa kuhudumia jamii ya wafanyabiashara ambao wapo masokoni hivyo ni vyema kila mfanyabiashara akaingizwa kwenye kanzidata hiyo ambapo itakuwa si rahisi kurudi tena barabarani.
Naye Mwenyekiti wa wafanyabiashara hao wilaya ya Ilala Saudi Mkupa, amesema kama serikali haitakuja na suluhu wafanyabiashara hao wataendelea kuondoka jambo ambalo sio dhamira ya serikali kwani serikali imekuwa na nia njema ya kuwasaidia wamachinga hapa nchini.