Wafanyabishara wakiwa katika kikao cha pamoja na maafisa kutoka Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Wafanyabiashara na baadhi ya wamiliki wa viwanda mkoani Mara wamelalamikia mfumo mbaya wa soko la bidhaa katika nchi jirani ya Kenya kwa kuweka vikwazo katika uuzaji wa bidhaa hatua ambayo imekuwa ikisabisha kero kubwa katika uuzaji wa bidhaa hizo zikiwemo za maziwa katika nchi hiyo.
Wakizungumza na ujumbe wa wizara ya ushirikiano wa Afrika Mashauriki ukiongozwa na naibu katibu mkuu wake Amantius Msole, wafanyabiashara hao wamesema kuwa licha ya vyombo vya dola nchini humo kuweka vikwazo katika uuzaji wa bidhaa nchini humo, wameiomba serikali kupunguza kodi kama zilivyo nchi wanachama hasa katika bidhaa ya maji safi ya kunywa ili kuwezesha bidhaa hizo kushindana katika soko.
Hata hivyo naibu katibu mkuu wa wizara ya ushirikiano wa Afrika Mashariki Amantius Msole, amesema lengo la ziara hiyo katika maeneo ya mipakani ni kuona jinsi watanzania wanavyonufaika na fursa ya soko la pamoja na changamoto zinazowakabili ili ziweze kupatiwa ufumbuzi.