Mtangazaji wa East Africa TV, Najma Paul akifurahi na wanafunzi wa Masasi baada ya kumaliza kugawa taulo za kike katika shule hiyo.
Septemba 19 kampeni ya Namthamini ilianza katika Wilaya ya Mtwara kwa kugawa taulo za kike katika shule ya sekondari Mikindani walioungana na wanafunzi kutoka shule ya Sekondari Mitengo, ambapo jumla ya pakiti 862 za taulo za kike zilitolewa kwa wanafunzi shule hizo mbili, pamoja na kutoa elimu ya hedhi salama kwa wanafunzi wa kike na kiume.
Pia katika siku hiyo kampeni ya Namthamini iliendelea katika shule ya Sekondari Naliendele walioungana na wanafunzi kutoka shule ya sekondari Mangamba, ambapo jumla ya taulo za kike pakiti 969 zilitolewa kwa wanafunzi wa shule zote mbili.
Septemba 20 kampeni ya Namthamini iliendelea katika wilaya ya Masasi ambapo ilifika katika shule tatu za sekondari nazo ni Chiungutwa, Lukuledi na Masasi ambapo jumla ya taulo za kike pakiti 3048 zilitolewa kwa shule hizo tatu.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Chiungutwa walipatiwa taulo za kike pakiti 1008
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Lukuledi walipatiwa taulo za kike pakiti 1056
Kampeni ya Namthamini wilaya ya Masasi ikamaliza kugawa taulo za kike katika wilaya hiyo katika shule ya Sekondari Masasi ambapo wanafunzi wa shule hiyo walipatiwa taulo za kike pakiti 984.
Septemba 21 kampeni ya Namthamini ikamaliza kugawa taulo za kike katika mkoa wa Mtwara katika wilaya ya Nanyumbu ambapo ilifika katika shule mbili za sekondari nazo ni Napacho na Nanyumbu.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Napacho ilipatiwa taulo za kike pakiti 1050.
Kampeni ya Namthamini katika mkoa wa Mtwara ikamaliza kugawa taulo za kike katika shule ya Sekondari Nanyumbu ambapo jumla ya taulo za kike pakiti 1008 zilitolewa katika shule hiyo.
Kampeni ya Namthamini itaendelea kugawa taulo za kike mwezi Oktoba katika mikoa ya Njombe na Ruvuma.