Wawakilishi wa vijana kutoka Afrika mashariki pamoja na balozi wa vijana katika jumuiya ya Madola kwa pamoja wamekutaka katika Kituo cha Maendeleo ya Kimataifa cha MS TCDC-USA RIVER Arusha.
Wawakilishi wa vijana kutoka Afrika Mashariki pamoja na balozi wa vijana katika Jumuiya ya Madola kwa pamoja wamekutana katika Kituo cha Maendeleo ya Kimataifa cha MS TCDC-USA RIVER Arusha katika ushirikishwaji mpana zaidi unaolenga kuwafanya vijana waweze kuwa sehemu ya kupanga na kufanya maamuzi katika kuitengeneza Jumuiya.
Akizungumza katika majadiliano hayo, Mkuu wa Wilaya ya Arusha Nyirembe Munasa ameonya dhana ya kuwachukulia Vijana kama bomu linalosubiri kulipuka na badala yake wafikiriwe kama rasilimali inayoweza kuijenga Afrika.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Vijana kutoka nchini Kenya Noli Kaaya amesema kuwa vijana wanaweza kuwa wawakilishi wazuri wa taifa katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo na uongozi katika kukuza uchumi.