
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma Ramadhan Kingai
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma Ramadhan Kingai amesema mwalimu huyo aliingiwa na tamaa ya ngono na ukatili wa kijinsia na kwamba mwalimu huyo, alikuwa akitumia madaraka yake kumlazimisha mwanafunzi huyo kila baada ya masomo ya jioni huku mwanafunzi huyo akilazimika kuchapwa viboko pindi anapomkatalia kufanya tendo hilo.
Wakati huo huo watu watatu wakazi wa Eneo la Murusi Kata ya Heruchini Wilayani Kasulu wamekamatwa na Polisi kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa Chuo cha Uuguzi Tanga mwaka wa kwanza kutokana na tamaa ya Ngono huku mwingine ambaye hajafahamika jina lake akiendelea kutafutwa baada ya kufanikiwa kutoroka.
Aidha katika Tukio nyingine, watu wawili wamekamatwa kwa kukutwa na Madawa ya Kulevya aina ya Bangi tani moja kitendo ambacho ni kinyume cha sheria.