Jumatano , 13th Jul , 2022

Endapo uchaguzi mkuu wa Kenya ungefanyika leo Julai 13, 2022, kusingekua na mbabe kutokana na washindani wawili wakubwa nchini humo Naibu Rais William Ruto na kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga kutofikia asilimia  50 ya kura kama katiba inavyotaka.

Kushoto ni William Ruto na kulia ni Raila Odinga

Bado wawili hao wanakimbizana kwenye matokeo ya tafiti mbalimbali zilifofanyika kwa wananchi ambapo Ruto ameachwa kwa asilimia chache na Odinga, huku  asilimia zote zikiwa chini ya 45%.

Takwimu mpya zilizotolewa mapema Jumatatu ya wiki hii zinaonyesha kuwa Muungano wa chama cha Azimio la Umoja cha mgombea Raila Odinga, bado unaongoza kwa kukubalika (japo kwa ushindi mwembamba ) dhidi ya kiongozi wa Kenya Kwanza Alliance, William Ruto.

Odinga anaongoza kwa 42 % wakati Naibu Rais Ruto akiwa nyuma yake kwa 39%.