Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Ramadhan Kingai
Kamanda Kingai amesema kwamba vijana wengi wamekuwa wakitumia ukuaji wa teknolojia ili kuleta suluhisho kwa vijana wengi kuondokana na dhana ya vijana kukaa mitaani na kujihusisha na uhalifu pamoja na madawa ya kulevya kwa kisingizio cha kukosa ajira.
Kamanda Kingai amesema program ya Drive Me, inalengo la kuanzisha kanzidata ya kuwapata madereva kwa wakati wowote, mahali popote weye weledi ambao wanaweza kutoa huduma kwa watu binafsi na hata kuwatumia kwenye shughuli kubwa za serikali ambazo zitahitaji kuajiri madereva wa muda.

