Jumatano , 20th Apr , 2022

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua kitabu cha Historia ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kitakachozinduliwa tarehe 26 Aprili, 2022 siku ya kilele cha Maadhimisho ya miaka 58 ya Muungano huo

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Selemani Jafo (kushoto) akizungumza wakati wa Mkutano ano na waandishi wa habari kuhusu Maadhimisho ya miaka 58 ya Muungano. Katikati ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, George Simbachawene na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi) – ZanzibarHamza Hassan Juma.

Baada ya uzinduzi, Ofisi ya Makamu wa Rais imepanga kuwa na mpango endelevu wa kutoa elimu kwa umma kuhusu historia ya Muungano na masuala ya msingi kuhusu Muungano

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Selemani Jafo amesema Muungano unapotimiza miaka 58 ni jambo la kujivunia na hatuna budi kuendeleza mazuri yaliyopatikana kutokana na Muungano na kusisitiza kuwa maadhimisho ya Muungano kwa mwaka huu yataambatana na matukio mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuelimisha umma kuhusu historia ya Muungano, tulipotoka, tulipo na tunapoelekea