Jumanne , 19th Apr , 2022

Serikali ya Uganda imetangaza kuwa hakuna mgonjwa wa Covid - 19 aliyelazwa hospitalini nchini humo
Msemaji wa wizara ya Afya Emmanuel Ainebyoona amesema pamoja na tangazo hilo wananchi waendelee kuchukua tahadhari zaidi.

Msemaji huyo anasema bado kuna baadhi ya watu wanaopima na kukutwa wameambukizwa lakini wapo katika hali nzuri isiyohitaji kulazwa Hospitalini.

Takwimu za hivi karibuni zinaonyesha kuwa kati ya Aprili 12 na Aprili 14, jumla ya kesi 27 zilipatikana. 
Dk Charles Olaro, mkurugenzi wa huduma za kliniki katika wizara ya Afya, wiki iliyopita alisema kulikuwa na wagonjwa wawili tu walio na Covid-19