
Wahamiaji hao watapewa hifadhi ya mpaka miaka 5 , ikiwemo kupewa mafunzo, malazi na huduma za afya.
Waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza Bi. Briti Patel alitembelea mji mkuu wa nchi hiyo Kigali ili kutia saini mkataba ulioitwa ushirikiano wa kiuchumi baina ya nchi hizo mbili.
Mpango huo utawafanya wahamiaji wanaoingia nchini Uingereza wakiwa kwenye boti ndogo, kusafirishawa moja kwa moja na serikali ya Uingereza kwa zaidi ya kilomita 6,400 kuelekea nchini Rwadna.
Rwanda imethibitisha kuhusu mkataba huo, lakini serikali zote mbili hazikutaka kuuelezea kwa undani.
Waziri wa mambo ya nje wa Rwanda Vincent Biruta, amesema kuwa mkataba huo utawapa wahamiaji nafasi ya kufanya maisha nchini Rwanda wakiwa kama raia kamili wa nchi hiyo.
Biruta ameongeza kuwa makubaliano hayo yatainufaisha Rwanda kimaendeleo
"Na wale ambao watakua hawatataka kuishi Rwanda, tutawarejesha makwao ," Biruta amesema.
Mahirika ya haki za binadamu yamekua yakikosoa utawala wa Rais Paul Kagame , lakini waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson, amesema kuwa nchi hiyo imeimarika sana katika miongo miwili iliyopita