Alhamisi , 14th Apr , 2022

Wizara ya TAMISEMI, imesahihisha taarifa yake iliyosomwa bungeni leo na Waziri wa Wizara hiyo Innocent Bashungwa na kusema kwamba, Pikipiki za maafisa ustawi wa jamii zilizonunuliwa zilikuwa ni 268.

Waziri wa TAMISEMI Innocent Bashungwa

Kupitia taarifa iliyotolewa leo Aprili 14, 2022, na Mkuu wa kitengo cha mawasiliano serikalini wa wizara hiyo imesema kwamba pikipiki hizo 268 zilinunuliwa kwa thamani ya shilingi milioni 789.9 na zilizosambazwa kwa awamu ya kwanza kwenye mamlaka za serikali za mitaa zilikuwa 68.