
Hassan Dilunga nyota wa Simba alipokuwa kwenye majukumu ya klabu yake.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika Klabu ya Simba, imeeleza kuwa nyota huyo ambaye aliwahi kuitumikia Yanga, ameondoka leo nchini akielekea Afrika Kusini.
Dilunga maarufu ''HD'' amekuwa nje ya dimba kuwa muda mrefu akiuguza jeraha ambalo limemfanya asiitumikie Simba kwa muda mrefu.
Nyota huyo alijiunga na Simba mwaka 2018 na kuwa sehemu ya mafanikio ya mataji mbalimbali waliyoyatwaa Simba kwa misimu miwili mfululizo.