
Ameeleza anataka kuonana na Cyril Ramaphosa kuzungumzia juu ya Vita vinavyowndelea nchini mwake huko mashariki mwa ulaya.
Balozi Liubov Abravitova amesema kuwa amelazimika kutumia mtandao wa Twitter kuomba kuonana na Rais baada ya mmalaka za nchi hiyo kumnyima kuonananae mara kadhaaa alipoomba wakutane.
Kupitia mtandao wa Twitter Balozi huyo amesema “Toka Urusi ivamie nchi yangu, sijaruhusiwa kabisa kuonana na Rais ama mawaziri wa Afrika Kusini, Watu wangu wanashambuliwa Sana na majeshi ya Russia" Balozi Abravitova ameandika.
Lakini Clayson Monyela, mmoja wa maafisa wa ngazi za juu ndani ya wizara ya mambo ya nje nchini Afrika Kusini, amekana shutuma hizo na kusema kuwa Balozi huyo alishapewa nafasi ya kuonana na baadhi ya maafisa wa serikali.