
Mbunge wa Iringa Mjini, Jesca Msambatavangu
Kauli hiyo ameitoa hii leo Aprili 14, 2022, Bungeni jijini Dodoma, wakati akitoa mchango wake na kusema athari inayotokea ni wanandoa kuachana na watoto kukosa malezi.
"Ukichukua takwimu hizo zinaonesha utaona wanaume wanashuka kwa sababu wao walikuwa juu zaidi kwenye kiwango cha kupiga na wanawake wanapanda kwa kasi kubwa, hii inaonesha ni namna gani sasa athari inaenda kuangukia kwa watoto," amesema Mbunge Jesca.