Alhamisi , 14th Apr , 2022

Kampuni ya Uber ambayo hutoa huduma ya usafiri ya taxi kwa njia ya mtandao imesitisha huduma zake nchini Tanzania kuanzia April 14 mwaka huu

Uber wanasema sababu kubwa kutokana na kuwepo kwa mazingira ambayo sio rafiki zinazosababisha changamoto kubwa katika uendeshaji wa biashara hiyo

“Kanuni za sasa za usimamizi wa sekta hii zimejenga mazingira ambayo si rafiki na zimekuwa changamoto kubwa katika uendeshaji wa biashara yetu, hadi pale muafaka utakapopatikana, hatutaendelea kutoa huduma za usafiri wa UberX, UberX Saver na UberXL nchini Tanzania” imeeleza taarifa ya kampuni hiyo