Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Ziporah Pangani.
Wakiongea kwa nyakati tofauti wananchi hao wamesema kukosekana kwa huduma ya nyama kumesabisha mambo mengi kwani sasa wamekuwa wakilazimika kununua samaki kwa gharama kubwa ambapo wameiomba serikali kukaa na wafanyabiashara hao kwa lengo la kutatua mgogoro huo
Mapema wakiongea mkoani hapo baadhi ya wafanyabiashara wa mifugo na nyama wamesema wao wataendelea kuonesha msimamo wao na kwamba endapo serikali ikishindwa kutatua mgororo huo kwa kutoruhusu bei ya nyama iuzwe kwa shilingi elfu tano, watalazimika kurudisha mifugo yao na kwenda kuiuza gulioni bila kuichinja.
Akiongea kwa njia ya simu Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Siporah Pangani amesema serikali itawaita wafanyabiashara hao kwa ajili ya kukaa pamoja na kuangalia namna ya kutatua mgogoro huo na amekili kwamba wananchi wamepata adha hiyo kwa siku mbili sasa hivyo serikali ina jukumu la kuhakikisha mgogoro huo unatatuliwa haraka ili wananchi waendele kupata huduma ya nyama kama kawaida.