Jumatatu , 28th Mar , 2022

Wakati zoezi la Sensa na Makazi nchini likitarajiwa kufanyika Agosti mwaka huu, Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Zanzibar (OCGS) imetoa tahadhari kwa wananchi kuepukana na matapeli waliojitokeza mitandaoni kutangaza nafasi za kazi za makarani.

Dkt. Albina Chuwa, Mtakwimu Mkuu wa Serikali

Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt Albina Chuwa amewambia waandishi wa habari kuwa kuna matapeli wamejitokeza na kusajili tovuti isiyo rasmi, huku baadhi ya watu wakiwa wameanza kujisajili kupitia tovuti hiyo batili.

Aidha Dkt Albina Chuwa amesema kwamba kazi ya kuwapata watumishi wa sense itasimamiwa na kamati za sense za mikoa ambazo wenyeviti wake ni Wakuu wa Mikoa husika.